skilleUnderholdning: Monsen (trippel)skille_slutt
Jul 2002 3_1
Her er du: NRK.no > Jul Sist oppdatert 11:58
KOLOFON
Publikum i NRK-studio? Send en epost til
---
Epost til redaksjonen:
---
Prosjektsjef for Radio- og Nett-underholdning
---
Vaktsjef og nettredaktør Underholdning:
 

Juleevangeliet på swahili


Publisert 28.12.2001 18:09. Oppdatert 29.11.2002 11:52.
02:01 Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote chini ya utawala wake wajiandikishe.
02:02 Kuandikishwa huku kulikuwa mara ya kwanza, wakati Kirenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria.
02:03 Basi, wote waliohusika walikwenda kujiandikisha, kila mtu katika mji wake.
02:04 Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya. Kwa kuwa alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yuda alikozaliwa Mfalme Daudi.
02:05 Alikwenda kujiandikisha pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mja mzito.
02:06 Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia,
02:07 akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.
02:08 Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao.
02:09 Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana.
02:10 Malaika akawaambia, "Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kuu kwa watu wote.
02:11 Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana.
02:12 Na hiki kitakuwa kitambulisho kwenu: mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini."
02:13 Mara kundi kubwa la jeshi la mbinguni likajiunga na huyo malaika, wakamsifu Mungu wakisema:
02:14 Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu aliopendezwa nao!
02:15 Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: "Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha."
02:16 Basi, wakaenda mbio, wakamkuta Maria na Yosefu na yule mtoto mchanga amelazwa horini.
02:17 Hao wachungaji walipomwona mtoto huyo wakawajulisha wote habari waliyokuwa wamesikia juu yake.
02:18 Wote waliosikia hayo walishangaa juu ya habari walizoambiwa na wachungaji.
02:19 Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake.
02:20 Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.

Siste saker:
Flere saker: ALT OM JULEEVANGELIET

 
Månetoppen
Copyright NRK © 2009  -  Telefon: 815 65 900  -  E-post: info@nrk.no